Publicidade

Salmos 51

4 Rum 3:4;Lk 15:21;Mwa 39:9Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,

Na kufanya maovu mbele za macho yako.

Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,

Na kuwa safi utoapo hukumu.

5 Ayu 14:4;Yn 3:6;Rum 5:12Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia;

Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi.

6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;

Nawe utanifundisha hekima kwa siri,

7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,

Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

8 Unifanye kusikia furaha na shangwe,

Mifupa uliyoiponda ifurahi.

9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;

Uzifute hatia zangu zote.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-