Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 56

Kumtumaini Mungu katika mateso

Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Njiwa Mkimya wa Mbali. Utenzi wa Daudi alipokamatwa na Wafilisti kule Gathi.

1 Zab 31:9 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,

Mchana kutwa ananionea akileta vita.

2 Zab 57:3 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,

Maana ni wengi wanaonipiga vita.

3 1 Sam 30:6;2 Nya 20:3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;

4 Ebr 13:5,6 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.

Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;

Mwenye mwili atanitenda nini?

5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,

Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.

6 Mdo 4:27,28 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,

Kwa kuwa waliniotea ili waniue.

7 Je! Wataokoka kwa uovu wao?

Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.

8 Mal 3:16 Umehesabu kutangatanga kwangu;

Uyatie machozi yangu katika chupa yako;

(Je! Hayamo katika kitabu chako?)

9 Isa 8:9,10 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.

Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;

10 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.

Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.

11 Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;

Mwanadamu atanitenda nini?

12 Zab 116:14-16 Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu;

Nitakutolea dhabihu za kushukuru.

13 Ayu 33:30 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti;

Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke?

Ili niende mbele za Mungu

Katika nuru ya walio hai.

Veja também