5 Mik 7:7,10Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu.
Maana tumaini langu hutoka kwake.
6 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika.
7 Yer 3:23Kwa Mungu wokovu wangu,
Na utukufu wangu;
Mwamba wa nguvu zangu,
Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
8 1 Sam 1:15;Zab 42:4Enyi watu, mtumainini sikuzote,
Ifunueni mioyo yenu mbele zake;
Mungu ndiye kimbilio letu.