Publicidade

Salmos 63

Faraja na uhakikisho katika Bwana

1 1 Sam 23:14Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,

Nafsi yangu inakuonea kiu,

Mwili wangu wakuonea shauku,

Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.

2 1 Nya 16:11Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,

Nizione nguvu zako na utukufu wako.

3 Yn 3:16Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;

Midomo yangu itakusifu.

4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;

Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.

5 Zab 17:15;Isa 25:6Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;

Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.

6 Zab 149:5Ninapokukumbuka kitandani mwangu,

Ninakutafakari usiku kucha.

7 2 Kor 1:10Maana Wewe umekuwa msaada wangu,

Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.

8 Isa 26:9Nafsi yangu inaambatana nawe sana;

Mkono wako wa kulia unanitegemeza.

9 Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiangamiza,

Wataingia katika vilindi vya nchi.

10 Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga,

Watakuwa riziki za mbwamwitu.

11 Sef 1:5Bali mfalme atamfurahia Mungu,

Kila aapaye kwa Yeye atashangilia,

Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-