Sifa kwa ajili ya wema wa Mungu kwa Israeli
1 Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
2 Imbeni utukufu wa jina lake,
Tukuzeni sifa zake.
3 Zab 18:44Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini!
Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako,
Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
4 Zab 67:3Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,
Naam, italiimbia jina lako.