Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1 Ee Mungu, tunakushukuru.
Tunakushukuru kwa kuwa Jina lako liko karibu;
Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu.
2 Nitakapoufikia wakati ulioamriwa,
Mimi nitahukumu hukumu za haki.
3 Ebr 1:3 Ingawa dunia na wote wakaao humo wataharuki,
Mimi mwenyewe nimezisimamisha nguzo zake.
4 Niliwaambia waliojivuna, Msijivune;
Na wasio haki, Msiiinue pembe.
5 Msiiinue pembe yenu juu,
Wala msinene kwa shingo ya kiburi.
6 Maana siko mashariki wala magharibi,
Wala nyikani itokako heshima.
7 1 Sam 2:7;2 Sam 5:2;Dan 2:21;Lk 1:52 Bali Mungu ndiye ahukumuye;
Humdhili huyu na kumwinua huyu.
8 Ayu 21:20;Yer 25:15;Ufu 14:10 Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe,
Na mvinyo yake inatoka povu;
Kumejaa machanganyiko;
Naye huyamimina.
Na sira zake wasio haki wa dunia
Watazifyonza na kuzinywa.
9 Bali mimi nitatangaza matendo yako milele,
Nitamwimbia Mungu wa Yakobo.
10 Nguvu zote za wasio haki nitazimaliza,
Lakini nguvu za mwenye haki nitaziimarisha.