Kwa mwimbishaji: kwa kufuata Yeduthuni. Ya Asafu. Zaburi.
1 Nimpazie Mungu sauti yangu,
Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.
2 Zab 50:15;Isa 26:9 Katika siku ya taabu yangu nilimtafuta Bwana;
Mkono wangu ulinyoshwa usiku, bila kulegea;
Nafsi yangu ilikataa kufarijika.
3 Nilipotaka kumkumbuka Mungu nilifadhaika;
Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.
4 Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike;
Nilitaabika nisiweze kunena.
5 Kum 32:7;Zab 14:5;Isa 51:9 Nilifikiri habari za siku za kale,
Miaka ya zamani zilizopita.
6 Nanena na moyo wangu usiku,
Nawaza moyoni mwangu,
Roho yangu naipeleleza.
7 Je! Bwana atatutupa milele na milele?
Asiwe na fadhili kwetu kamwe?
8 Isa 27:11;Yon 2:4;Hes 23:19;Yer 15:18;Rum 9:6 Rehema zake zimekoma hata milele?
Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote?
9 Isa 49:15 Mungu amesahau fadhili zake?
Amezuia kwa hasira rehema zake?
10 Ayu 42:3;Zab 31:22;Yer 10:19 Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo;
Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu.
11 1 Nya 16:12;Zab 28:5;Isa 5:1 Nitayakumbuka matendo ya BWANA;
Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.
12 Pia nitaitafakari kazi yako yote;
Nitaziwaza habari za matendo yako.
13 Zab 73:17 Ee Mungu, njia yako iko katika utakatifu;
Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?
14 Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;
Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.
15 Kwa mkono wako umewakomboa watu wako,
Wana wa Yakobo na Yusufu.
16 Kut 14:21;Yos 3:15,16 Ee Mungu, yale maji yalikuona,
Yale maji yalikuona, yakaogopa.
Vilindi vya maji navyo vikatetemeka,
17 Mawingu yakamwaga maji.
Mbingu nazo zikatoa sauti,
Mishale yako nayo ikatapakaa.
18 Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli;
Umeme uliuangaza ulimwengu.
Nchi ilitetemeka na kutikisika;
19 Hab 3:15;Kut 14:28;Ayu 37:23 Njia yako ilikuwa katika bahari.
Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu;
Hatua zako hazikujulikana.
20 Isa 63:11 Uliwaongoza watu wako kama kundi,
Kwa mkono wa Musa na Haruni.