Wema wa Mungu na Israeli kukosa shukrani
1 Kut 19:5;Kum 32:29Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu,
Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu.
2 Zab 49:4;Mt 13:35Nitafumbua kinywa changu kwa mithali,
Niyatamke mafumbo ya kale.
3 Zab 44:1Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu,
Ambayo baba zetu walituambia.
4 Kum 4:9;Kut 12:26;Yos 4:6,7Hayo hatutawaficha wana wao,
Huku tukiwaambia kizazi kingine,
Sifa za BWANA, na nguvu zake,
Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.