Publicidade

Salmos 82

Ombi la kupata haki

Zaburi ya Asafu.

1 Mhu 5:8;Kut 21:6 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;

Katikati ya miungu anahukumu.

2 Kum 1:17;Zab 58:1,2 Hadi lini mtahukumu kwa dhuluma,

Na kuzikubali nyuso za wabaya?

3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima;

Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara;

4 Mwokoeni maskini na mhitaji;

Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.

5 Zab 11:3 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;

Misingi yote ya nchi imetikisika.

6 Ayu 21:32;Eze 31:14;Yn 10:34 Mimi nimesema, Ndinyi miungu,

Na wana wa Aliye Juu, enyi nyote.

7 Lakini mtakufa kama wanadamu,

Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.

8 Zab 2:8;Ufu 11:15 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi,

Maana mataifa yote ni yako.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-