Publicidade

Salmos 95

Mwito wa kuabudu na kutii

1 Njoni, tumwimbie BWANA,

Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.

2 Tuje mbele zake kwa shukrani,

Tumfanyie shangwe kwa zaburi.

3 Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,

Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.

4 Mkononi mwake zimo bonde za dunia,

Hata vilele vya milima ni vyake.

5 Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,

Na mikono yake iliumba nchi kavu.

6 1 Fal 8:54;1 Nya 6:13;Ezr 9:5;Dan 6:10;Lk 22:41;Mdo 7:60;1 Kor 6:20;Efe 3:14;Ayu 35:10;Isa 54:5;Yn 1:3 Njoni, tuabudu, tusujudu,

Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

7 Ebr 3:7-11,15;4:7;Zab 95:7-11;Hes 14:22 Kwa maana ndiye Mungu wetu,

Na sisi tu watu wa malisho yake,

Na kondoo za mkono wake.

Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!

8 Kut 17:1-7;Hes 20:2-13 Msifanye mioyo yenu kuwa migumu;

Kama ilivyokuwa huko Meriba

Kama siku ile katika Masa jangwani.

9 Hapo waliponijaribu baba zenu,

Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

10 Ebr 3:10 Miaka arubaini nilichukizwa na kizazi kile,

Nikasema, Hawa ni watu wenye mioyo inayopotoka,

Na wanaopuuza njia zangu.

11 Hes 14:20-23;Kum 1:34-36;12:9-10;Ebr 4:3,5 Ndipo Nikaapa kwa hasira yangu

Hawataingia katika pumziko langu.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_23-13-58-