Sifa kwa Mungu atoaye hukumu
1 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Mwimbieni BWANA, nchi yote.
2 Mwimbieni BWANA, lisifuni jina lake,
Tangazeni wokovu wake kila siku.
3 Wahubirieni mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
4 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana.
Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
5 Isa 41:24;Yer 10:11;Hab 2:18-20;Mdo 19:26;1 Kor 8:4,5;Mwa 1:1;Isa 42:5;Yer 10:11Maana miungu yote ya watu si kitu,
Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
6 Heshima na adhama ziko mbele zake,
Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
7 Zab 29:1-2Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
8 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake,
Leteni sadaka, na mwingie katika nyua zake.
9 Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu,
Tetemekeni mbele zake, nchi yote.