Shukrani kwa wema wa Mungu
1 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 Isa 33:24;Mt 9:2;Mk 2:5;Lk 7:47;Kut 15:26;Yer 17:14Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
4 Aukomboa uhai wako kutoka kwa kaburi,
Akutia taji la fadhili na rehema,