1 1 Nya 16:18,34;2 Nya 5:13;7:3;Ezr 3:11;Zab 100:5;106:1;107:1;136:1;Yer 33:11 Haleluya.
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Zab 115:9 Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3 Mlango wa Haruni na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4 Wamchao BWANA na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5 Zab 18:19 Katika shida yangu nilimwita BWANA;
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6 Ebr 13:6;Rum 8:31 BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;
Mwanadamu atanitenda nini?
7 Zab 54:4 BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,
Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wakiwa wameshindwa.
8 Zab 62:8;Isa 2:22;Yer 17:5,7 Ni heri kumkimbilia BWANA
Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9 Zab 146:3;Isa 30:2,3 Ni heri kumkimbilia BWANA.
Kuliko kuwatumainia wakuu.
10 Mataifa yote walinizunguka;
Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
11 Zab 88:17 Walinizunguka, naam, walinizunguka;
Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
12 Kum 1:44;Mhu 7:6 Walinizunguka kama nyuki,
Walizimika kama moto wa miibani;
Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
13 Ulinisukuma sana ili nianguke;
Lakini BWANA akanisaidia.
14 Kut 15:2;Isa 12:2 BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu,
Naye amekuwa wokovu wangu.
15 Sauti ya furaha na wokovu
Imo hemani mwao wenye haki;
Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.
16 Kut 15:6 Mkono wa kulia wa BWANA umetukuzwa;
Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.
17 Zab 6:5;73:28 Sitakufa bali nitaishi,
Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
18 Mit 3:11,12;1 Kor 11:32 BWANA ameniadhibu sana,
Lakini hakuniacha nife.
19 Isa 26:2 Nifungulieni malango ya haki,
Nitaingia na kumshukuru BWANA.
20 Zab 24:7;Isa 35:8 Lango hili ni la BWANA,
Wenye haki ndio watakaoliingia.
21 Nitakushukuru kwa maana umenijibu,
Nawe umekuwa wokovu wangu.
22 Mt 21:42;Mk 12:10;Lk 20:17;Mdo 4:11;Efe 2:20;1 Pet 2:4,7 Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.Mt 21:42;Mk 12:10-11
23 Ayu 5:9 Neno hili limetoka kwa BWANA,
Nalo ni ajabu machoni petu.
24 2 Kor 6:2 Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,
Tutashangilia na kuifurahia.
25 Mt 21:9;Mk 11:9;Yn 12:13 Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;
Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.
26 Zek 4:7;Mt 21:9;23:39;Mk 11:9;Lk 13:35;19:38;Yn 12:13 Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;
Tumewabariki toka nyumbani mwa BWANA.
27 Est 8:16;Mik 7:9;Mal 4:2 BWANA ndiye aliye Mungu,
Naye ndiye aliyetupa nuru.
Ifungeni dhabihu kwa kamba
Pembeni mwa madhabahu.
28 Kut 15:2;Isa 25:1 Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru,
Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.
29 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.