Shukrani kwa ukombozi wa Israeli
Wimbo wa kupanda mlima.
1 Mwa 15:1;Hes 14:9;Yos 1:5;Ebr 13:5;Rum 8:31 Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,
Israeli na aseme sasa,
2 Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,
Wanadamu walipotushambulia.
3 Zab 35:25;Mit 1:12;Yer 51:34 Papo hapo wangalitumeza hai,
Hasira yao ilipowaka juu yetu.
4 Papo hapo maji yangalitugharikisha,
Mto ungalipita juu ya roho zetu;
5 Papo hapo maji yafurikayo
Yangalipita juu yetu.
6 Na ahimidiwe BWANA;
Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.
7 Nafsi yetu imeokoka kama ndege
Katika mtego wa wawindaji,
Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.
8 Kut 18:4;Zab 12:2;Mit 18:10;Isa 50:10;Ebr 13:6 Msaada wetu u katika jina la BWANA,
Aliyeziumba mbingu na nchi.