Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 125

Usalama wa watu wa Mungu

Wimbo wa kupanda mlima.

1 Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,

Ambao hautikisiki, wakaa milele.

2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,

Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,

Tangu sasa na hata milele.

3 Kwa maana fimbo ya udhalimu

Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki;

Ili wenye haki wasije wakainyosha

Mikono yao kwenye upotovu.

4 Ee BWANA, uwatendee mema walio wema,

Nao walio wanyofu wa moyo.

5 Mit 2:15;Isa 59:8;Flp 2:15;Gal 6:16 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka,

BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu.

Amani ikae na Israeli.

Veja também