Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 13

Sala ya ukombozi kutoka kwa adui

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Kum 31:17;Ayu 13:24;Zab 22:1;Isa 59:2 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele?

Hadi lini utanificha uso wako?

2 Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini,

Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?

Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?

3 Ezr 9:8;Zab 18:28;Lk 2:32;Ufu 21:23;Zab 76:5,6;Isa 37:36;Yer 51:39;Efe 5:14 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;

Uyatie nuru macho yangu,

Nisije nikalala usingizi wa mauti.

4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;

Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.

5 2 Nya 20:12 Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako;

Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.

6 Naam, nitamwimbia BWANA,

Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

Veja também