Shangwe kwa kusamehewa
1 Rum 4:7-8;Zab 85:2Heri aliyesamehewa dhambi,
Na kuondolewa makosa yake.
2 Law 17:4;Rum 5:13;Yn 1:47;2 Kor 1:12Heri ambaye BWANA hamhesabii hatia,
Na ambaye rohoni mwake hamna hila.
3 Nilipokosa kuungama dhambi zangu, mifupa yangu ilipooza
Kwa kulia kwangu mchana kutwa.
4 Kwa maana mchana na usiku
Mkono wako ulinilemea.
Jasho langu likakauka hata nikawa
Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 Mit 28:13;Isa 65:24;Lk 15:18Ndipo nikakuungamia dhambi yangu,
Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,
Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
6 1 Tim 1:16;Isa 55:6;Yn 7:34Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye
Akuombe awapo katika dhiki.
Hakika maji makuu yafurikapo,
Hayatamfikia yeye.