Sifa kwa kukombolewa katika shida
1 1 Sam 21:13-15Nitamhimidi BWANA kila wakati,
Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
2 Yer 9:24;1 Kor 1:31Katika BWANA nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie na kufurahi.
3 Mtukuzeni BWANA pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.