2 Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka?
Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?
4 Efe 4:26;Mit 3:7Muwe na hofu wala msitende dhambi,
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
6 Zab 80:3Wengi husema, Nani atakayetuonesha mema?
BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.
7 Umenitia furaha moyoni mwangu,
Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
8 Law 26:5;Kum 12:10;Yn 14:27;Flp 4:7Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,
Maana Wewe, BWANA, peke yako,
Ndiwe unijaliaye kukaa salama.