2 Eze 36:25;Zek 13:1;1 Kor 6:11;Ebr 9:14;1 Yoh 1:7;Ufu 1:5Unioshe kabisa uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu.
3 Zab 32:5Maana nimejua mimi makosa yangu
Na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
4 Rum 3:4;Lk 15:21;Mwa 39:9Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,
Na kufanya maovu mbele za macho yako.
Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,
Na kuwa safi utoapo hukumu.