Publicidade

Salmos 80

Sala ya kurejeshwa kwa Israeli

Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yungiyungi, Agano. Ya Asafu. Zaburi.

1 Kut 25:22;Kum 33:2;1 Sam 4:4;Zab 89:1 Wewe uchungaye Israeli, usikie,

Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi;

Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.

2 Mbele ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,

Uziamshe nguvu zako,

Uje, utuokoe.

3 1 Fal 18:37 Ee Mungu, uturudishe,

Uangaze uso wako nasi tutaokoka.

4 Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hadi lini

Utayaghadhibikia maombi ya watu wako?

5 Umewalisha mkate wa machozi,

Umewanywesha machozi kwa kipimo kikuu.

6 Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu,

Na adui zetu wanacheka wao kwa wao.

7 Ee Mungu wa majeshi, uturudishe,

Uangaze uso wako nasi tutaokoka.

8 Isa 5:1,7;Yer 2:21;Eze 15:6 Ulileta mzabibu kutoka Misri,

Ukawafukuza mataifa ukaupanda.

9 Ulitengeneza nafasi mbele yake,

Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi.

10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,

Matawi yake ni kama mierezi ya Mungu.

11 Kut 23:31;Zab 72:8 Nao uliyaeneza matawi yake hadi baharini,

Na vichipukizi vyake hadi kunako Mto.

12 Isa 5:5 Kwa nini umezibomoa kuta zake,

Wakauchuma wote wapitao njiani?

13 Nguruwe wa msituni wanauharibu,

Na hayawani wa kondeni wanautafuna.

14 Zek 1:12,16,17;Isa 63:15 Ee Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,

Utazame toka juu uone, uujie mzabibu huu.

15 Isa 49:5 Na mche ule ulioupanda

Kwa mkono wako wa kulia;

Na tawi lile ulilolifanya

Kuwa imara kwa nafsi yako.

16 Umechomwa moto; umekatwa;

Kwa lawama ya uso wako wanapotea.

17 Zab 89:21;Kut 4:22;Zab 110:1;Dan 7:13,14;Yn 5:21-27 Mkono wako na uwe juu yake

Mtu aliye katika mkono wako wa kulia;

Juu ya mwanadamu uliyeimarisha

Kwa nafsi yako;

18 Kisha hatutakuacha kwa kurudi nyuma;

Utuhuishe nasi tutaliitia jina lako.

19 Hes 6:25;Zab 27:4,9 Ee BWANA, Mungu wa majeshi, uturudishe,

Uangaze uso wako nasi tutaokoka.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_23-13-58-