Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 86

Maombi ya kutaka msaada juu ya watesi

Sala ya Daudi

1 Ee BWANA, utege sikio lako unijibu,

Maana mimi ni maskini na mhitaji.

2 Unihifadhi nafsi yangu,

Maana mimi ni mcha Mungu.

Wewe uliye Mungu wangu,

Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini.

3 Wewe, Bwana, unifadhili,

Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.

4 Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,

Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.

5 Zab 130:7-8;Yoe 2:13 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,

Umekuwa tayari kusamehe,

Na mwingi wa fadhili,

Kwa watu wote wakuitao.

6 Ee BWANA, uyasikie maombi yangu;

Uisikilize sauti ya dua zangu.

7 Siku ya mateso yangu nitakuita,

Kwa maana utaniitikia.

8 Kut 15:11;Kum 3:24;1 Sam 2:2;2 Sam 7:22;1 Fal 8:23 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana,

Wala matendo mfano wa matendo yako.

9 Zab 95:6-7;Isa 43:7;Ufu 15:4 Mataifa yote uliyoyaumba watakuja;

Watakusujudia Wewe, Bwana,

Watalitukuza jina lako;

10 Kum 6:4;Isa 37:16;Mk 12:29;1 Kor 8:4;Efe 4:6 Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,

Wewe ndiwe mfanya miujiza,

Ndiwe Mungu peke yako.

11 Ee BWANA, unifundishe njia yako;

Nitakwenda katika kweli yako;

Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;

12 Nitakusifu Wewe, Ee Bwana, Mungu wangu,

Kwa moyo wangu wote,

Nitalitukuza jina lako milele.

13 Zab 56:13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana;

Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.

14 Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia;

Kundi la watu wakatili wanataka kuniua.

Wala hawakukuweka Wewe

Mbele ya macho yao.

15 Kut 34:6;Hes 14:18;Neh 9:17;Yoe 2:13;Zab 103:8;111:4 Lakini Wewe, Bwana,

U Mungu wa rehema na neema,

Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.

16 Unielekee na kunifadhili mimi;

Mpe mtumishi wako nguvu zako,

Umwokoe mwana wa mjakazi wako.

17 Unifanyie ishara ya wema,

Wanichukiao waione na kuaibishwa.

Kwa kuwa Wewe, BWANA,

Umenisaidia na kunifariji.

Veja também