Hakikisho la ulinzi wa Mungu
1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
4 Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.