Publicidade

Salmos 93

Ukuu wa enzi ya Mungu

1 Isa 52:7;Ufu 19:6;Ayu 40:10;Zab 104:1;Isa 59:17 BWANA ametamalaki, amejivika adhama,

BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme.

Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

2 Mit 8:22 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;

Wewe ndiwe uliye tangu milele.

3 Ee BWANA, mito imepaza,

Mito imepaza sauti zake,

Mito imepaza uvumi wake.

4 Zab 29:10 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu,

Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo,

BWANA Aliye Juu ndiye mwenye ukuu.

5 Shuhuda zako ni amini sana;

Utakatifu ndio uifaao nyumba yako,

Ee BWANA, milele na milele.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-