Mwito wa kuabudu na kutii
1 Njoni, tumwimbie BWANA,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
2 Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
3 Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,
Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4 Mkononi mwake zimo bonde za dunia,
Hata vilele vya milima ni vyake.
5 Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na mikono yake iliumba nchi kavu.
6 1 Fal 8:54;1 Nya 6:13;Ezr 9:5;Dan 6:10;Lk 22:41;Mdo 7:60;1 Kor 6:20;Efe 3:14;Ayu 35:10;Isa 54:5;Yn 1:3Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.