Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 103

8 Kut 34:6;Hes 14:18;Kum 5:10;Yak 5:11BWANA amejaa huruma na neema,

Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

9 Isa 57:16;Yer 3:5;Mik 7:18Yeye hatashutumu daima,

Wala hatashika hasira yake milele.

10 Ezr 9:13Hakututenda kulingana na hatia zetu,

Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.

11 Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,

Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.

12 Isa 43:25;Efe 1:7Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Veja também